• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaipongeza Burkina Faso kukata "uhusiano wa kibalozi" na Taiwan

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:41:03

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lu Kang amesema China inapongeza uamuzi wa Burkina Faso kukata "uhusiano wa kibalozi" na Taiwan.

    Bw. Lu amesema inajulikana duniani kuwa mwezi Oktoba mwaka 1971, kikao cha 26 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilipitisha Azimio Nambari 2758 na kuweka bayana kuwa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China.

    Ameongeza kuwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu utafanya ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili ufikie kwenye ngazi mpya.

    Amesema China inaikaribisha Burkina Faso kujiunga na ushirikiano huo mapema iwezekanavyo, kwenye msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako