• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 49 wafariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama DRC

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:41:28

    Watu wasiopungua 49 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Mto Kongo, kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Gavana wa mkoa wa Tshuapa Bw. Mboyo Iluka amesema boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka kijiji cha Monkoto kuelekea Mbandaka imezama na chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

    Tume inayoundwa na maofisa waandamizi wa mkoa huo imepelekwa kwenye eneo la ajali kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

    Ajali katika Mto Congo huwa zinasababishwa na hali mbaya za boti au boti kubeba abiria kupita kiasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako