• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaahidi kutunga sheria mpya kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:41:54

    Kenya itatunga sera na sheria kuboresha huduma kwa watu milioni 3.5 wenye ulemavu nchini humo.

    Waziri wa kazi na ulinzi wa kijamii wa Kenya Bw. Ukur Yatani amesema serikali kuu na serikali ya kaunti zote zimekubali kufanya suala la ulemavu kuwa ajenda kuu katika kutunga sera, ili kuhimiza ukuaji shirikishi na umoja. Ameongeza kuwa Kenya inakaribia kukamilisha utungaji wa sera ya walemavu ya kitaifa na katiba mpya pia itahimiza haki na huduma kwa watu wenye ulemavu.

    Bw. Yatani amesema hayo mjini Nairobi kabla ya mkutano wa kilele kuhusu walemavu duniani utakaoandaliwa kwa pamoja na serikali za Kenya na Uingereza tarehe 24, Julai mjini London.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako