• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yatoa mwito kusitisha mapambano kaskazini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-05-25 14:26:51

    Jumuiya ya kimataifa imeonyesha wasiwasi juu ya mapambano yaliyoibuka upya kati ya vikosi vya Somaliland na Puntland pembezoni mwa mji wa Tukaraq mkoani Sool.

    Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, shirika la IGAD, Marekani na nchi nyingine, zimezihimiza pande hizo mbili zisitishe mapambano mara moja na kuanzisha mazungumzo kati ya makamanda wa majeshi kwenye eneo hilo, kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu waliopoteza makazi, na kufanya mazungumzo kuhusu mgawanyo wa majeshi na kubadilishana askari wa usalama waliofungwa.

    Mapambano kati ya pande hizo mbili yanatokea wakati hali ya kibinadamu ni ngumu, kutokana na madhara yaliyosababishwa na kimbunga cha Sagar.

    Majimbo hayo mawili ya Somalia yamekuwa yakipambana tangu mwaka 2002 kuhusu udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako