• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa majaji wakuu wa Mahakama Makuu wa shirika la SCO wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-05-25 17:32:35

    Mkutano wa 13 wa majaji wakuu wa Mahakama kuu wa Nchi wanachama wa Shirika la ushirikiano la Shanghai SCO umefanyika leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwa kwa mkutano huo. Pia ameeleza kuwa mkutano huo ukiwa utaratibu muhimu wa ushirikiano wa sheria wa shirika la SCO, umetoa mchango muhimu katika kuimarisha wazo la ujenzi wa sheria, mawasiliano kuhusu mifumo ya sheria, na kukuza ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali kati ya nchi wanachama wa shirika hilo. Rais Xi amesema anatumai kuwa majaji hao wataendeleza ushirikiano wa sheria chini ya mfumo wa SCO, kupambana na uhalifu na kuondoa migogoro kwa hatua zenye ufanisi, ili kuweka mazingira mazuri ya sheria katika kuhimiza maendeleo ya kikanda ya shirika hilo.

    Tokea utaratibu wa mkutano wa majaji wakuu wa Mahakama kuu za nchi wanachama wa SCO ulipoanzishwa mwaka 2006, mahakama kuu za nchi mbalimbali wanachama wa SCO zimepata mafanikio katika kupambana kwa pamoja na uhalifu wa kuvuka mipaka, kutatua kwa mashauriano migogoro mbalimbali ya biashara, hali ambayo imechangia katika kuhimiza ujenzi wa mambo ya sheria, kulinda amani na utulivu wa kikanda na kuboresha mazingira ya uendeshaji wa biashara.

    Mbali na majaji wakuu kutoka nchi wanachama wa SCO, mkutano huo kwa mara ya kwanza umewaalika majaji wakuu wa mahakama makuu za nchi waangalizi wa SCO pamoja na wenzi wa mazungumzo ya shirika hilo, pande mbalimbali zimefanya majadiliano kwa kina kuhusu masuala ya kupambana na ugaidi, dawa za kulenvya na magendo ya fedha.

    Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Guo Shenkun ametoa mapendekezo matatu kuhusu nchi mbalimbali kuanzisha ushirikiano wa sheria ulio wa karibu, ufanisi mkubwa zaidi:

    "Inapaswa kukuza ushirikiano wa sheria kuhusu usalama wa kikanda kwa kufuata mtizamo wa usalama wa pamoja, shirikishi, ushirikiano na maendeleo endelevu; kukuza ushirikiano wa sheria kwa kufuata wazo la biashara huria na yenye ufanisi mkubwa zaidi na kukuza ushirikiano wa habari na mawasiliano kuhusu sheria ya kikanda."

    Jaji mkuu wa Mahakama kuu ya Russia Bw. Vyacheslav amesema Russia imefanya juhudi kubwa katika kukamilisha utaratibu wa sheria, pia anatumai kuwa nchi mbalimbali zilizoshiriki kwenye mkutano huo zitaimarisha uratibu na ushirikiano wakati wa kufanya ushirikiano wa sheria wa kuvuka mipaka ya nchi. Mbali na hayo anaona kuwa kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia moja" kunahitaji pande mbalimbali kuweka kwa pamoja mazingira mazuri ya sheria. Anasema:

    "Russia inaunga mkono kujenga mazingira mazuri ya sheria katika hatua ya ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', pia inaona kuwa katika mchakato huo inapaswa kuweka msingi wa pamoja wa sheria."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako