• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema China ni mfano mzuri wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-05-25 18:41:02

    Katibu mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Bibi Patricia Espinosa amesema katika miaka ya karibuni, China imekuwa na jukumu muhimu katika mchakato wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bi. Patricia amesema hayo hapa Beijing. Amesema anaamini kuwa ushiriki wa China ni sababu muhimu ya kufikiwa kwa makubaliano ya Paris, na kwamba China imechukua hatua nyingi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ambazo zinaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, kutunga sera zinazofaa kuboresha viwango vya afya na maisha ya watu, kukuza maendeleo ya uchumi, na kuwa mfano kwa nchi zote.

    Katika mchakato huu, China imetoa fursa na mawazo mapya mengi ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako