• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano watokota kati ya mikoa ya Geita na Mwanza kuhusu usafirishaji wa madini

    (GMT+08:00) 2018-05-25 20:27:45

    Mvutano wa kimasilahi umeibuka baina ya mikoa ya Geita na Mwanza nchini Tanzania baada ya mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel kupiga marufuku usafirishwaji wa madini ghafi (cabon) kutoka mkoani humo kwenda jijini Mwanza.

    Kufuatia hatua hiyo, mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella amesema biashara na masuala ya kiuchumi hayawezi kuwekewa mipaka ya kimkoa, bali kinachotakiwa ni shughuli hizo kuzingatia sheria na kanuni ikiwemo malipo ya ushuru na kodi.

    Kwa upande wake, Gabriel amepiga marufuku uchenjuaji wa madini nje ya Mkoa wa Geita akieleza kuwa nia yake ni kubakiza fursa za ajira mkoani humo na utajiri kuunufaisha mkoa huo.

    Mkuu huyo wa mkoa ametangaza Mei 31 kuwa siku ya mwisho kwa cabon yenye madini ya dhahabu kusafirishwa na kuchenjuliwa nje ya Geita, huku wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vya uchenjuaji wakitakiwa kufungua au kuvihamishia mkoani Geita.

    Hata hivyo, Mongella amesema anaamini hakuna mgogoro utakaoibuka kati ya Serikali, wafanyabishara na wamiliki wa viwanda vya uchenjuaji kwa sababu lengo kuu la makundi yote ni ujenzi wa uchumi na maendeleo ya wananchi.

    Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda vya Uchenjuaji wa Dhahabu Mkoa wa Mwanza, George Onyango amesema wamemwandikia barua Mongella kumuomba aingilie kati suala hilo kwa kuwasiliana na mwenzake wa Geita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako