• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakubali walaghai walilipwa mabilioni ya fedha

    (GMT+08:00) 2018-05-25 20:28:04

    Serikali imekubali kuwa wafanyabiashara walaghai walilipwa mabilioni ya fedha baada ya kuwasilisha mahindikwa halmashauri ya nafaka na mazao NCPB badala ya wakulima halisi. Huku sakata hiyo ikiendelea kutokota, katibu wa wizara ya kilimo Bw Richard Lesiyampe amesema NCPB tayari imewalipa wafanyabiashara hao zaidi ya shilingi bilkionbi 1.5 kutokana na shilingi bilioni 8.7 zilizopaswa kulipwa wakulima halisi. Hata hivyo katibu huyo ameshikilia kuwa hakuna fedha zilizopotea katika sakata hiyo akisema mahindi yote yaliwasilishwa katika NCPB. Bodi hiyo ilianza kununua mahindi kutoka kwa wakulima Octoba mwaka jana kwa bei ya shilingi 3,200 kwa gunia la kilo 90. Hivi sasa NCPB ina jumla ya magunia ya mahindi milioni 3.8 maghala yake kote nchini Kenya.Kauli yake inawiana na ile ya waziri wa kilimo BwMwangi Kiunjurialiyewataka wakenya kutokuwa na wasiwasi kwa sababu serikali haikupoteza pesa zoizote katika shughuli ya ununuzi wa mahindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako