• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaadhimisha siku ya 55 ya Afrika

  (GMT+08:00) 2018-05-26 16:52:12

  Maadhimisho ya siku ya 55 ya Afrika yamefanyika jana hapa Beijing. China imezipongeza nchi za Afrika kutokana na mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyopatikana kufuatia kuimarika kwa umoja na ushirikiano baina ya zenyewe kwa zenyewe, na ikiahidi kuwa itaendelea kuwa mshiriki muhimu na wa kufaa katika maendeleo ya bara la Afrika.

  Balozi wa Madagascar nchini China, ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa mabalozi wa nchi za Afrika Bw. Victor Sikonina amesisitiza umuhimu wa kufanya maadhimisho ya siku ya Afrika. Anasema,

  "Siku ya Afrika imetupa fursa ya kujulisha Bara la Afrika linaloendelea kwa kasi. Afrika imaamua kuwa nguvu muhimu ya kimataifa, inajitahidi kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo uhifadhi wa mazingira, uhamiaji wa watu, ugaidi, usalama wa chakula, afya, na maendeleo endelevu."

  Naye balozi wa Rwanda nchini China Bw. Crispus Kiyonga amesema Afrika inatilia maanani ushirikiano wa kimataifa haswa ushirikiano na China. anasema,

  "Tukikosa uungaji mkono wa wenzi wetu wa kimataifa, hatutapata mafanikio katika utandawazi na maendeleo ya uchumi. Ushirikiano kati ya Afrika na China ni muhimu sana, tunapaswa kuongeza zaidi ushirikiano huo."

  Alipohutubia maadhimisho hayo, naibu spika wa bunge la umma la China Bw. Cao Jianming amesema, China na Afrika zina maslahi na majukumu ya pamoja, na ni jumuiya yenye muskabali wa pamoja. Anasema,

  "Hivi sasa kwa mujibu wa mawazo ya rais Xi Jinping ya ujamaa wenye umaalumu wa China, China inajitahidi kusukuma mbele ujenzi wa uhusiano mpya wa kimataifa na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Katika mchakato huu, China na nchi za Afrika zinatakiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako