• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai kuwa Marekani na Korea Kaskazini zitamaliza tofauti zao

    (GMT+08:00) 2018-05-26 18:19:50

    China imesema, ina matumaini kuwa Korea Kaskazini DPRK na Marekani zitatunza maendeleo ya sasa ili kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo na kusukuma mbele mchakato wa kuifanya Peninsula ya Korea kuwa sehemu isiyokuwa na silaha za nyuklia.

    Taarifa imetolewa jana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Lu Kang wakati akijibu swali kuhusu maoni ya China baada ya Rais Donald Trump kutangaza kufuta mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini.

    Akijibu swali kuhusu hatua ya DPRK kubomoa vituo vya majaribio ya nyuklia, Bw. Lu amesema ilikuwa hatua muhimu iliyopigwa na DPRK kuacha matumizi ya nyuklia na ilikuwa muhimu kwa mchakato wa kuifanya Peninsula ya Korea kuwa sehemu isiyokuwa na silaha za nyuklia.

    Katika hatua nyingine Rais Trump jana amesema Marekani huenda ikatangaza tena kufanya mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

    Trump amesema mazungumzo kwa ajili ya hilo yanaendelea baina ya Marekani na DPRK kuona kama itafaa kufanya mkutano huo kwa kuwa nchi zote mbili zinaonyesha nia ya kukutana.

    Mpaka sasa Naibu wa kwanza wa Waziri wa mambo ya nje wa Korea Bw. Kim Kye Gwan amesema nchi yake iko tayari kukaa chini na Marekani muda wowote katika namna yoyote ili kujadili jinsi ya kumaliza tofauti zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako