• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China apongeza uzinduzi wa Maonyesho ya mwaka 2018 ya kimataifa ya viwanda vya Big Data ya China

    (GMT+08:00) 2018-05-26 18:21:09

    Maonyesho ya mwaka 2018 ya kimataifa ya viwanda vya Big Data ya China imefunguliwa leo mjini Guiyang, mkoani Guizhou. Rais Xi Jinping wa China ametoa barua za pongezi kwa uzinduzi wa maonyesho hayo.

    Kwenye barua hiyo, rais Xi amesema kuwa, hivi sasa teknolojia mpya ya mawasiliano ya habari kama vile mtandao wa Internet, Big Data na AI zimepata maendeleo makubwa, na kuleta athari kubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii, utawala wa taifa, usimamizi wa jamii na maisha ya watu wa nchi mbalimbali. Kutumia vizuri fursa ya maendeleo ya Big Data, kuhimiza maendeleo mazuri ya viwanda vya Big Data, na kushughulikia changamoto za usalama wa data na usimamizi wa mtandao wa Internet, kunahitaji nchi mbalimbali kuimarisha maingiliano na ushirikiano. Pia amesisitiza kuwa, China inazingatia maendeleo ya Big Data. Anatumai wajumbe wanaohudhuria maonyesho hayo kujadiliana kwa kina, kushirikiana kuhimiza maendeleo ya uvumbuzi wa Big Data, kujenga maisha yenye busara, kunufaisha watu wa nchi mbalimbali na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako