• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU waadhimisha Siku ya Afrika kwa kurudia wito wa kuongeza juhudi za kuondoa ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-05-26 18:23:24

    Umoja wa Afrika jana umeadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuanzishwa kwa uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika OAU, na kurudia tena wito wa kupiga vita dhidi ya ufisadi.

    Sherehe ya kumbukumbu ya miaka 55 ya AU katika makao makuu ya jumuiya hiyo ya nchi za Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, ilikwenda sambamba na mkutano wa majadiliano, maonyesho ya mavazi na bidhaa za kitamaduni za nchi wanachama na onyesho la muziki.

    Akizungumzia mafanikio ya Afrika katika nyanja tofauti, mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Afrika, Mousa Faki Mahmat, alisema kuna uhitaji wa kuwa waangalifu na kufahamu kuwa bado kuna kazi ya kupambana na vizuizi vinavyokwamisha juhudi za kujiendeleza.

    Amesema kazi kubwa iliyopo mbele ni kupambana na ufisadi katika hali zake zote, akisisitiza kwamba rushwa inaharibu maisha ya watu wa kawaida na inashusha uaminifu kwa viongozi wao na kwenye taasisi za umma katika barani Afrika.

    AU imeutangza mwaka 2018, kuwa mwaka wa mapambano dhidi ya rushwa, ukiwa na kauli isemayo, " kushinda vita dhidi ya Ufisadi: ndio njia endelevu ya mageuzi ya Afrika", na viongozi wa Afrika walitangaza kuwa kila tarehe 11 mwezi Julai kila mwaka itakuwa ni siku ya mapambano dhidi ya ufisadi, na Rais wa Nigeria ametangazwa kuwa mshindi katika kutekeleza kauli mbiu hiyo ya kupambana na ufisadi, ikiwa ni kutokana na msimamo wa utawala wake katika kupambana na rushwa nchini Nigeria na duniani kote.

    Umoja wa nchi Huru za Afrika (OAU) ulianzishwa mnamo Mei 25 mwaka 1963, kwa mkataba uliosainiwa na nchi 32 wanachama, na baadaye mwaka 2002 umoja huo ukabadilishwa jina kuwa Umoja wa nchi za Afrika, na sasa una nchi wanachama 55.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako