• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mataifa makubwa yakutana kujadili jinsi ya kuisaidia Iran

    (GMT+08:00) 2018-05-26 18:51:42

    Baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran, mataifa makubwa matano yamekutana siku ya ijumaa mjini Vienna nchini Austria ili kujadili, na yakiwa na imani kubwa ya kufanikiwa.

    Pia ulikuwa ndiyo mkutano wa kwanza kati ya China, Russia, Uingereza, Ujerumani na Irani kwa lengo la kusaidia suala la Iran baada ya Marekani kujitoa.

    Ili kutatua suala hilo, pande zote zinahitaji kutafuta njia ili kuendeleza mchakato wa utekelezaji, ikiwemo kusimamia vituo vya nyuklia vya Iran, huku hatua mbadala zikitafutwa ili kulinda maslahi ya kiuchumi ya Iran. Kutokana na hali ya vikwazo vilivyowekwa na Marekani, kazi hiyo inapata ugumu.

    Akizungumza na waandishi wa habari, naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran, Bw. Abbas Araghchi amesema sasa ana matumaini baada ya mkutano huo wa nchi tano, licha ya kuwa hakukuwa na azimio lililotolewa isipokuwa nchi hizo zimepeana majukumu ya utekelezaji.

    Aidha Bw. Abbas amesema nchi yake inasubiri fidia iliyopendekezwa na kuona kama ufumbuzi utapatikana juu ya suala la Iran.

    Iran pia imetoa pendekezo la kufanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje mapema ili kusukuma zaidi mchakato wa kujadili utatuzi wa suala lake, na pendekezo hilo lilikubaliwa na nchi hizo tano licha ya kuwa tarehe kamili haikutangazwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako