• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump anaangalia uwezekano wa kufanyika mkutano kati ya Marekani na DPRK Juni 12

    (GMT+08:00) 2018-05-27 16:41:02

    Rais wa Marekani jana alisema anaangalia uwezekano wa kufanya mkutano na kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwezi Juni 12 mwaka huu.

    Trump amesema majadiliano kuhusu mkutano huo ambao unapangwa kufanyika nchini Singapore, yanaendelea vizuri jambo alilosema linaleta matumaini kuwa huenda ukafanyika.

    Alhamisi iliyopita Rais Trump alitangaza kufuta mkutano akisema ni ngumu kufanyika kutokana na chuki na uhasama wa wazi ulioonyeshwa na Korea Kaskazini kupitia matamko yake ya hivi karibuni.

    Habari nyingine zinasema, viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini jana wamekutana tena katika sehemu ya Panmun, wakieleza matumaini ya pamoja ya kuboresha uhusiano kati ya pande hizo mbili na kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako