• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafuriko nchini Somalia yaua watu 21, na maelfu kuyakimbia makazi yao

    (GMT+08:00) 2018-05-27 16:43:29

    Takribani watu 21 wamefariki na wengine maelfu wameathirika kufuatia mafuriko na dhoruba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha sehemu mbalimbali nchini Somalia.

    Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya haki za binadamu OCHA, ya mjini Mogadishu imesema mafuriko na dhoruba hiyo vimeathiri watu karibia 800,000 na wengine zaidi ya 230,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao, pia vimeathiri makazi ya watu, mifugo na hata miundo mbinu mingi ya msingi katika nchi hiyo.

    Taarifa hiyo ya OCHA, pia inaeleza kuwa kati ya watu hao 21 waliofariki, 9 ni kutoka jimbo la Hirshabelle, 4 kutoka Jubalanda na 8 wa kutoka mkoa wa Banadir.

    Aidha, serikali ya Somalia pamoja na washirika wake wa misaada ya kibinadamu inatafuta fedha dola za kimarekani milioni 80 kukabiliana na athari zilizoletwa na mafuriko na kusababisha idadi kubwa ya wahitaji wa misaada ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako