• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasifu Burkina Faso kutoa uamuzi sahihi wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2018-05-27 17:56:46

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Alpha Barry na kusaini taarifa ya pamoja ya kurejesha uhusiano wa kibalozi kati ya China na Burkina Faso.

    Bw. Wang Yi amesema kuwa, China inasifu serikali ya Burkina Faso kufuata mkondo wa zama hizi na kufanya uamuzi sahihi wa kisiasa. Amesema kuwa, kuwepo kwa China moja ni kanuni ya uhusiano wa kimataifa inayokubaliwa na jumuiya ya kimataifa, pia ni msingi wa kisiasa wa China kuendeleza uhusiano na nchi yoyote.

    Pia amesema rais Xi Jinping wa China anakaribisha rais Christian Kabore wa Burkina Faso kuhudhuria mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini Beijing mwezi Septemba, na rais Kabore ameeleza matarajio yake ya kuhudhuria mkutano huo na kujadiliana na rais Xi Jinping kuhusu mambo makuu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Burkina Faso, na kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako