• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasema vikwazo vinavyowekwa na Mrekani dhidi yake vinakwamisha mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2018-05-27 18:19:40

    Sudan Kusini imesema vikwazo vinavyowekwa na Marekani dhidi yake vinapelekea waasi kushindwa kushiriki mazungumzo ya amani.

    Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, balozi wa Sudan Kusini nchini Ethiopia na kwa Umoja wa Afrika, Bw. James Morgan, amesema Marekani kuingia kwa mfumo wa kuzuia usafirishaji wa silaha, na kuwawekea vikwazo maofisa wa serikali ya Sudan Kusini kumesababisha upatikanaji wa amani Sudan Kusini kuwa ngumu.

    Balozi Morgan amesema serikali yake iko tayari kupokea mapendekezo ambayo yanaendana na matakwa ya katika ya Sudan Kusini, pia akisema serikali hiyo iko tayari kupokea mapendekezo ambayo yataondoa mvutano uliopo dhidi ya waasi, akitolea mfano muundo wa jeshi na mfumo wa uwakilishi bungeni.

    Taarifa hii ya Balozi Morgan imekuja muda mfupi baada ya mazungumzo ya hivi karibuni kuhusu amani ya Sudan Kusini kushindwa kupatikana makubaliano baina ya pande mbili zinazohasimiana.

    Tangu hapo awali nchi hiyo iliingia kwenye machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi, kulifanya kuwa moja ya eneo lenye janga la wakimbizi linalokuwa kwa kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako