• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yafanya maombolezo ya kitaifa ya waganda 22 walipoteza maisha kwenye ajali ya barabarani

    (GMT+08:00) 2018-05-28 09:16:03

    Serikali ya Uganda imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu, baada ya watu 22 kupoteza maisha yao kwenye ajali ya barabarani iliyotokea ijumaa usiku magharibi mwa nchi hiyo.

    Waziri Mkuu wa Uganda Bw. Ruhakana Rugunda amesema Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameagiza bendera ya taifa kwenye majengo yote ya umma kupepea nusu mlingoti kuanzia jana. Pia amesema serikali itatoa msaada wa dola 1,400 kwa kila familia kwa ajili ya mazishi ya waliofariki.

    Katika ajali hiyo basi la abiria liligonga trekta na lori la bia na kusababisha vifo vya watu 19 papo hapo na wengine wawili walifariki wakiwa njiani kwenda hospitali.

    Kila mwaka Uganda inakuwa na ajali karibu elfu 20 zinazosababisha vifo vya watu elfu mbili kwa wastani, na kuifanya kuwa moja ya nchi zenye ajali nyingi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako