• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duque, Petro kushindana kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais Colombia

    (GMT+08:00) 2018-05-28 09:18:32

    Bw. Ivan Duque, mgombea urais wa chama cha mrengo wa kulia wa DCP amepata ushindi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Jumapili, kwa kupata asilimia zaidi ya 39 ya kura. Kutokana na kuwa hajapata zaidi ya nusu ya kura kama inavyohitajika kisheria, Bw. Duque atapambana tena na mgombea wa chama cha mrengo wa kushoto Bw. Gustavo Petro kwenye duru ya pili ya upigaji kura itakayofanyika Juni 17. Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika baada ya serikali ya Colombia kusaini makubaliano ya kihistoria na kundi la upinzani la FARC, na kukomesha mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako