• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadudu waharibu hekta elfu 17 za mazao Wilayani Kilosa, Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-05-28 09:38:26

    Ofisa wa kilimo wa wilaya ya Kilosa, Mkoa Morogoro Bibi Tatu Kachenje, amesema wadudu wameharibu zaidi hekta elfu 17 za mazao ya chakula na biashara.

    Bibi Kachenje amesema viwavi jeshi, panya na ndege aina ya kwerea kwerea wameshambulia zaidi mashamba ya mahindi, mpunga na pamba. Amesema kuna wasiwasi kuwa kata 27 za wilaya hiyo zitakumbwa na uhaba wa chakula katika miezi ijayo.

    Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na wadau wengine imekuwa inaendelea kuwaelimisha wakulima namna ya kuwatambua na kuwadhibiti wadudu hao.

    Viwavi jeshi ni wadudu wanaokula kila mmea wanaokutana nao. Asili ya wadudu hao ni Amerika ya Kusini, lakini mwaka 2016 waligunduliwa nchini Nigeria na wamekuwa wakisambaa kwenye nchi nyingine za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako