• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema mwafaka wa kimataifa juu ya makubaliano ya nyuklia yanaitenga Marekani

    (GMT+08:00) 2018-05-28 10:02:16

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amesema nchi nyingi duniani isipokuwa Israel na nchi kadhaa za kiarabu zimeeleza kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran ambayo Marekani imejitoa.

    Amesema rais Donald Trump wa Marekani ameshindwa kubadilisha mwafaka wa kimataifa wa kuunga mkono makubaliano hayo.

    Akizungumzia majadiliano yanayoendelea kati ya Iran na nchi nyingine 5 zinazohusika na makubaliano hayo, Bw. Zarif amesema Iran itaendelea kuyatekeleza makubaliano hayo kama maslahi yake yanaweza kutimizwa na kulindwa.

    Pia ameongeza kuwa Marekani itajitenga yenyewe kutoka jumuiya ya kimataifa kutokana na mikakati yake mipya ya kukabiliana na Iran.

    Ijumaa iliyopita, naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Abbas Araqchi alikutana na wenzake kutoka Ulaya, Russia na China kujadili hatma ya makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako