• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Asaidia timu yake kufuzu michuano ya Yuropa

  (GMT+08:00) 2018-05-28 10:08:22

  Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta jana usiku ameisaidia timu yake, KRC Genk kupata tiketi ya kucheza michuano ya ligi ya Europa baada ya kufunga goli moja kati ya mawili ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu Zulte Waregem.

  Samata ambaye ni Nahodha huyo wa Timu ya taifa ya Tanzania, alifunga goli lake hilo kunako dakika ya 18, kabla ya mchezaji mwingine wa timu hiyo Jere Uronen kufunga la pili dakika ya 28.

  Kwa Genk kufuzu michuano ya Ligi ya Europa mwakani, hii inakuwa ni mara ya tatu mfululizo kwa Samatta kucheza michuano hiyo tangu ajiiunge na timu hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako