• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Taifa la Libya laweka masharti ya kushiriki kwenye mkutano wa Paris

    (GMT+08:00) 2018-05-28 10:24:33

    Baraza la Juu la Taifa la Libya limeweka masharti ya kushiriki kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Libya unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ambao utafanyika kesho mjini Paris.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya habari ya Baraza hilo imesema Baraza hilo limepiga kura kuidhinisha kutuma ujumbe mjini Paris, huku likisisitiza msimamo thabiti kuwa makubaliano ya kisiasa ni utaratibu pekee halali unaoambatana na pendekezo lililotolewa na Ufaransa.

    Taarifa imeongeza kuwa chaguzi zinatakiwa kufanywa baada ya kura za maoni kuhusu katiba, ili kuelekea kwenye kipindi cha kudumu, na kwamba serikali ya Libya inatakiwa kuwa ya kiraia, na kazi za taasisi za jeshi na usalama zinatakiwa kusimamiwa na serikali hiyo ya kiraia.

    Baraza pia limetaka kusimamishwa mara moja kwa vita katika mji wa mashariki wa Darna, ambao umeshuhudia mapigano tangu mwezi Februari kati ya jeshi la Libya mashariki mwa nchi na wapiganaji wanaodhibiti mji huo.

    Wiki mbili zilizopita, Ufaransa ilitoa pendekezo kwa pande za kisiasa za Libya kufanya mkutano mjini Paris, kujadili mpango wa Ufaransa wenye lengo la kumaliza mgogoro wa kisiasa wa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako