• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai kufanyika mjini Qingdao, China

  (GMT+08:00) 2018-05-28 17:33:50

  Waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi leo hapa Beijing ametangaza kuwa, mkutano wa 18 wa kamati ya utendaji ya viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai utafanyika mjini Qingdao, China kuanzia tarehe 9 hadi 10 mwezi ujao, na rais Xi Jinping wa China ataendesha mkutano huo.

  Huu ni mkutano wa kwanza wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai tangu jumuiya hiyo ipanuliwe. Bw. Wang Yi amesema mkutano huo utahudhuriwa viongozi wa nchi wanachama 8, na nchi 4 waangalizi wa jumuiya hiyo na wakuu wa mashirika ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa. Anasema,

  "Rais Xi ataandaa dhifa kwa ajili wageni, na kuendesha mazungumzo, na kubadilishana nao maoni kuhusu hali ya sasa na mustakabali wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai, ushirikiano katika nyanja mbalimbali kutokana na hali mpya duniani, na masuala muhimu ya kikanda na kimataifa, ili kuhimiza jumuiya hiyo itoe mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya kikanda."

  Katika mwaka mmoja uliopita tangu mkutano wa kilele uliofanyika mwaka jana mjini Astana, Kazakhstan, China imeandaa mikutano na shughuli kubwa za pande mbalimbali zaidi ya 160 kwa kufuata mfumo wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai. Mikutano na shughuli hizo zimehimiza uaminifu wa kisiasa, ushirikiano halisi na mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi wanachama. Katika mkutano utakaofanyika mjini Qingdao, rais Xi pamoja na viongozi wengine watasaini Taarifa ya Qingdao. Bw. Wang anasema,

  "Mkutano huo utatoa Taarifa ya Qingdao, ambalo litajumuisha uzoefu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai katika miaka 17 iliyopita, kueneza uaminifu, usawa, kunufaishana, kujadiliana, kuheshimiana na kushirikiana ili kukabiliana kwa pamoja mabadiliko yenye utatanishi duniani."

  Aidha, mkutano huo pia utapitisha mwongozo wa utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano wa kirafiki wa ujirani mwema wa muda mrefu kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai katika miaka mitano ijayo, mwongozo wa ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi, ufarakanishaji na msimamo mkali wa kidini katika miaka mitatu ijayo, na makubaliano kadhaa kuhusu ushirikiano katika sekta za forodha, kilimo, uhifadhi wa mazingira na utalii. Bw. Wang anasema,

  "Mkutano wa kilele wa Qingdao utatoa sauti kubwa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo uendeshaji wa mambo ya kimataifa, na kuimarisha utaratibu wa biashara wa pande mbalimbali, kutetea mawazo ya maendeleo yanayozingatia uvumbuzi, uratibu, uhifadhi wa mazingira, kufungua mlango, na kunufaishana, ili kutoa mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai. Mkutano huo pia utahimiza pande mbalimbali kuunganisha zaidi mkakati wa maendeleo, na kutengeneza injini ya maendeleo ya pamoja, haswa kusukuma mbele pendekezo la 'Ukanda Mmoja na Njia Moja', ili kuinua kiwango cha ushirikiano wa kikanda wa uchumi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako