• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kuijengea China kuwa nchi kubwa ya teknolojia duniani

    (GMT+08:00) 2018-05-28 18:33:38

    Mkutano wa 19 wa wanataaluma wa Akademia ya Sayansi na mkutano wa 14 wa wanataaluma wa akademia ya uhandisi ya China umefunguliwa leo hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano huo akisisitiza kuwa, China ikitaka kustawi, ni lazima kujitahidi kuendeleza sayansi na teknolojia, na kuifanya China iwe kituo muhimu cha sayansi na uvumbuzi. Amesema wadau wa sayansi na teknolojia wa China wanapaswa kutambua hali ya jumla, kutumia fursa, kukabiliana na matatizo mbalimbali, na kulenga maendeleo mapya ya sayansi na teknolojia ya dunia. Pia kuongoza mwelekeo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, na kubeba majukumu ya kihistoria ya kuwa waongozaji wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya zama mpya.

    Rais Xi pia amesema, wanataaluma wanapaswa kushiriki kwa kina kwenye usimamizi wa sayansi na teknolojia ya dunia, kuchangia busara ya China, na kutia mkazo katika kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako