• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kongamano la kimataifa la kupambana na ugaidi ya "Ukuta Mkuu –mwaka 2018" lafunguliwa hapa Beijing

  (GMT+08:00) 2018-05-28 20:28:08

  Kongamano la polisi wa kimataifa la kupambana na ugaidi la "Ukuta Mkuu-mwaka 2018" limefunguliwa leo asubuhi hapa Beijing, na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi 180 wa jeshi la polisi kutoka nchi 28.

  Akihutubia ufunguzi huo, Naibu mkuu wa Jeshi la polisi nchini China Jenerali Qin Tian amesema kongamano hilo linalenga kujenga jukwaa la ushirikiano, kubadilishana mbinu za kupata mafanikio, kuinua uwezo wa kukabiliana na matukio ya ugaidi kwa pamoja, na kulinda usalama wa taifa na utulivu wa jamii wa nchi mbalimbali. Amesema China inapinga kithabiti aina zote za ugaidi, na inatafuta kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi na jumuiya ya kimataifa na kufanya juhudi kuchangia katika kulinda amani na utulivu wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako