• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Iraq lapitisha kuhesabiwa upya kwa asilimia 10 ya kura kutokana na tuhuma za udanganyifu

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:08:16

    Bunge la Iraq limeitisha kikao cha dharura na kupitisha uamuzi wa kuhesabiwa upya kwa asilimia 10 ya kura kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika Mai 12, kutokana na tuhuma za kuwepo wa vitendo vya udanganyifu, kugushi, na kukiuka kanuni. Taarifa iliyotolewa na bunge hilo inasema kama robo ya kura kati ya asilimia hiyo 10 zikikutwa na udanganyifu, kura zote za uchaguzi huo zitahesabiwa upya, na kura zilizokusanywa kutoka nje ya nchi zitabatilishwa. Mai 19, Tume ya uchaguzi ya Iraq ilitangaza kuwa muungano unaoongozwa na imam wa madhehebu ya Shia Moqtada al-Sadr umepata ushindi kwenye uchaguzi huo kwa kupata viti 54 kati ya vyote 329 bungeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako