• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji kupitia upya sheria ya ndoa ili kupambana na ndoa za utotoni

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:15:52

    Bunge la Msumbiji limetangaza kuwa linajiandaa kuondoa kipengele kimoja kwenye sheria ya familia, kinachoruhusu wasichana kuolewa wakiwa na miaka 16 kama wazazi wao wanaridhika.

    Msemaji wa bunge la Msumbiji Bibi Veronica Macamo amesema bunge kwa sasa linafikiria kufanya umri huo kuwa miaka 18, na uamuzi huo unatokana na ongezeko la kasi la ndoa za utotoni, na malalamiko kutoka kwa jumuiya za kiraia kuwa kipengele hicho cha sheria ya familia kinakiuka haki za watoto.

    Bunge pia lilijadili hatma ya wanafunzi wanaopata uja uzito shuleni na kuamua waendelee kusoma katika madarasa yao, uamuzi ambao baadhi ya wazazi wameupinga, wanafunzi wenyewe hawajafurahishwa nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako