• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yatoa mwito wa ushirikiano katika kupambana na vurugu za kijinsia

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:16:14

    Mwito umetolewa kwa jamii nchini Afrika Kusini kuungana kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kufuatia tukio la hivi karibuni la wasichana wawili wanafunzi kunyongwa.

    Wasichana hao walikutwa wamenyongwa bwenini kwao katika jimbo la Kaskazini magharibi. Inaaminika kuwa wasichana hao walinyongwa na mvulana mwenye umri wa miaka 19, aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wasichana hao. Kijana huyo amekamatwa na uchunguzi unaendelea.

    Waziri wa elimu ya msingi wa Afrika Kusini Bibi Angie Motshekga, amesema jamii inatakiwa kutuma ujumbe kuwa wasichana sio takataka na haki inatakiwa kutendeka kwa wanaofanya ukatili kama huo dhidi ya wanawake. Tukio hili linafuatilia tukio la hivi karibuni la msichana mmoja mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Mangosuthu kuuawa na aliyekuwa mpenzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako