• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanne wauawa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:28:57

    Kamanda wa polisi jimbo la Borno, Nigeria Bw. Damian Chukwu, amesema watu wanne wameuawa, na wengine saba wamejeruhiwa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga lililofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram kwenye mji wa Konduga, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

    Kamanda Chukwu ameongeza kuwa washambuliaji waliingia kwenye kijiji cha Mashimari, eneo la Konduga, karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani, na kufanya shambulizi hilo.

    Kundi la Boko Haram linatuhumiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20,000 na wengine milioni 2.3 kukimbia makazi yao, tangu lianze operesheni zake mwaka 2009.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako