• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga shutuma za Marekani kuhusu uhamisho wa teknolojia

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:51:27

    Balozi wa China katika Shirika la biashara duniani WTO Bw. Zhang Xiangchen amepinga shutuma za Marekani kuwa China imetumia vibaya makubaliano ya mahitaji ya ubia na kuchukua teknolojia, akisema Marekani ni nchi inayonufaika zaidi kutokana na uhamishaji wa teknolojia.

    Akiongea kwenye mkutano wa WTO kuhusu utatuzi wa migogoro DSB, Bw. Zhang ameeleza kuwa teknolojia zinazohamishwa kutoka kampuni za Marekani kwa kampuni za China ni shughuli za kawaida zinazofanyika kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande mbili, pamoja na matakwa ya kampuni, hatua ambayo inafuata kanuni za biashara huria na ushindani kwenye soko.

    Pia amesisitiza kuwa ukaguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani hauwezi kutoa ushahidi kuthibitisha kuwa sheria za China zinayalazimisha makampuni ya kigeni kutoa teknolojia kwa washirika wake wa China, wala haukutoa ushahidi kwamba China imekiuka kanuni za WTO kwa kuweka utoaji wa teknolojia kama sharti kwa uwekezaji wa kigeni kuingia nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako