• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yatarajia kukamilisha ujenzi wa barabara zenye kilomita laki mbili ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:59:05

    Serikali ya Ethiopia imesema inapanga kujenga mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita laki mbili ndani ya miaka miwili.

    Mamlaka ya barabara ya Ethiopia imetoa ripoti ikisema serikali inatarajia kukamilisha ujenzi huo kabla ya muda wa Mpango wa pili wa miaka mitano wa Maendeleo na Mageuzi kwisha mwaka 2020, ambao urefu wa barabara unatarajiwa kuwa maradufu kuliko ule uliomalizika katika mpango wa kwanza wa miaka mitano.

    Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kwa sasa Ethiopia ina barabara zenye urefu wa zaidi ya kilometa laki 1.2 zikiwa ni pamoja na barabara za changarawe, na lengo la kuwa na kilometa laki 2 litatimizwa. Katika muda wa miaka 27 iliyopita, urefu wa barabara nchini Ethiopia umeongezeka kutoka kilometa elfu 19 hadi kilometa laki 1.13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako