• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria kuwarudisha nyumbani magaidi 105 wa Mali

    (GMT+08:00) 2018-05-29 09:59:26

    Algeria itawarudisha nyumbani magaidi 105 wa Mali, waliokamatwa na vikosi vya kupambana na ugaidi vya Algeria katika mikoa mitano iliyo kusini mwa nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa ofisa usalama aliyenukuliwa na Gazeti la El Watan la Algeria, magaidi hao walikamatwa kutokana na kujenga kambi za mafunzo nchini Algeria ili kutoa mafunzo kwa kundi la wapiganaji la Mali Ansar Eddine. Ofisa huyo amesisitiza kuwa magaidi hao wanashikiliwa na kuorodheshwa kuwa watu hatari ambao wanatakiwa kurudishwa nyumbani chini ya ulinzi mkali.

    Algeria imeamua kuwarudisha watu hao mjini Bamako kwa ndege baada ya kushauriana na ubalozi wa Mali mjini Algiers.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako