• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Afrika Kusini kupewa mafunzo nchini China kuhusu maeneo maalumu ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-05-29 10:00:07

    Jumla ya wadau 50 wa maeneo maalumu ya kiuchumi kutoka Afrika Kusini watapewa mafunzo katika sekta hiyo nchini China kuanzia Mei, 31 hadi Juni, 7.

    Maofisa hao kutoka Idara ya Biashara na Viwanda ya Afrika Kusini, idara za majimbo na manispaa pamoja na mashirika yanayowajibika na utekelezaji wa maeneo maalumu ya kiuchumi watashiriki kwenye mpango huo wa kujenga uwezo kuhusu sekta hiyo mjini Tianjin.

    Naibu waziri wa biashara na viwanda Bw. Bulelani Magwanishe amesema wadau hao watapata mafunzo ya kiufundi kuhusu kupanga, kuendeleza, kusimamia na kuendesha maeneo maalumu ya kiuchumi, utaalamu ambao ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya maeneo hayo nchini Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako