• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Baiskeli, Cameroun: Timu ya taifa ya Rwanda yaingia tano bora siku ya pili

    (GMT+08:00) 2018-05-29 10:09:36

    Bonaventure Uwizeyimana wa timu ya taifa ya Rwanda jana amefanikiwa kukamata nafasi ya tano kwenye hatua ya pili ya mashindano ya mbio za baiskeli ya kimataifa yanayoendelea nchini Cameroun.

    Katika hatua hiyo ya pili yenye umbali wa kilomita 175.7 kutoka mji wa Kribi hadi mjini Douala, mwendesha baiskeli Noel Richet wa Ufaransa alikamata nafasi ya kwanza.

    Waendesha baiskeli wengine kutoka timu ya Rwanda katika hatua hiyo, Patrick Byukusenge alikamata nafasi ya 9, Didier Munyaneza ya 10, Jean Paul Rene Ukiniwabo 24, Janvier Hadi 27 na Jean Bosco Nsengimana aliyekamata nafasi ya 40.

    Mashindano hayo yanendelea leo kwa hatua ya tatu yenye urefu wa kilomita 108 ndani ya mji wa Douala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako