• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Mechi ya Kirafiki Kimataifa: Kenya yaishinda Equatorial Guinea

    (GMT+08:00) 2018-05-29 10:10:48

    Mchezaji Pistone Mutamba jana amefunga goli la ushindi wa 1-0 iliopata timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) kwenye mechi ya kirafiki dhidi Equatorial Guinea iliyopigwa kwenye uwanja wa Kenyatta katika County ya Machakos.

    Pistone alifunga goli hilo katika dakika ya 73 akiunganisha pasi iliyopigwa na Ovella Ochieng na kuipa ushindi wa kwanza timu hiyo chini ya kocha mpya Sebastien Migne.

    Mechi ni ya pili kwa kocha Migne kufanya majaribio ya kikosi chake alichokifanyia mabadiliko, ambapo katika mechi ya kwanza Kenya ilifungwa na Swaziland kwa goli 1-0 katika uwanja huo huo wa Machakos.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako