• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina nia na uwezo wa kutoa mchango zaidi kwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-05-29 10:12:01

    Usalama na maendeleo na changamoto mbili za kimsingi zinazokabili Afrika. Kutokana na kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya maendeleo na kuongezeka kwa nguvu za taifa la China, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta ya usalama umekuwa sehemu muhimu ya uhusiano wa aina mpya wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika. Kabla ya kuwadia kwa Siku ya Kimataifa ya Walinzi Amani wa Umoja wa Mataifa, mkurugenzi wa kituo cha ushirikiano wa usalama cha ofisi ya ushirikiano wa kijeshi wa kimataifa iliyo chini ya Wizara ya Ulinzi ya China Bw. Zhou Bo amesema China ina nia na uwezo wa kutoa mchango kwa ushirikiano wa amani na usalama kati ya China na Afrika, pamoja na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

    Mwaka 2015, Septemba, rais wa China alitoa ahadi kubwa kwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa kilele wa ulinzi amani wa Umoja wa Mataifa. Ahadi ambazo ni pamoja na kuunda jeshi la kuwa tayari lenye watu elfu 8, kutoa mafunzo kwa walinzi amani elfu 2 wa nchi nyingine, na kutoa msaada wa kijeshi wa dola za kimarekani milioni 100 kwa Umoja wa Afrika. Baada ya juhudi za miaka miwili, China imepata maendeleo makubwa katika kutekeleza ahadi hizo. Bw. Zhou anasema,

    "Mwaka jana tulikamilisha mchakato wa kuandikisha kikosi chenye askari elfu nane katika Umoja wa mataifa, wakiwemo wanajeshi 850 wa China watakaoshiriki kwenye maandalizi ya kikosi cha mbele cha Umoja wa mataifa yenye askari elfu nne, ambao inawezekana kuwa watatumwa kwenye maeneo yenye migogoro ndani ya siku 60, na kupewa majukumu magumu na yenye hatari kubwa. Mpaka sasa tumetoa mafunzo kwa askari 1,600 kati ya 2,000 kama tulivyoahidi. Kwa upande wa misaada ya kijeshi ya bila malipo kwa Afrika, hivi sasa tunafanya mazungumzo na Umoja na mataifa na misaada hiyo itatolewa kama ilivyoahidiwa."

    Ikiwa nchi kubwa inayowajibika, China imeshiriki kwa muda mrefu kwenye shughuli za kimataifa za kulinda amani zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa. Hivi sasa, China imekuwa moja ya nguvu kuu za utaratibu wa kulinda amani wa Afrika. Kwa mujibu wa Bw. Zhou, China imetuma walinzi amani nchini Sudan, Sudan Kusini, Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lebanon, ambapo shughuli nyingi za ulinzi amani zinafanywa barani Afrika.

    "China na Umoja wa Afrika zina uhusiano mzuri, China inatekeleza majukumu ya kulinda amani barani Afrika kwa njia mbili, kwanza ni kutuma vikosi kwenye maeneo yenye migogoro; Pili, tunatoa misaada ya usalama kwa nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika. Kwa mfano, zamani China iliwahi kutoa misaada ya kijeshi kwa Burundi na Uganda, ili kuwasaidia kutekeleza majukumu ya kulinda amani nchini Somalia. Hii pia ni moja ya njia za kutoa misaada. Aidha, pia tunafanya majadiliano moja kwa moja na Umoja wa Afrika, na kuwaacha waamue ni maeneo gani yanahitaji zaidi misaada yetu."

    Bw. Zhou pia amesema kutokana na mabadiliko ya hali, majukumu yanayoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwa walinzi amani yanaongezeka siku hadi siku. Kwa mfano wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wanabeba majukumu 11 ikiwemo kusimamia usimamishaji wa vita, zoezi la uchaguzi na kuhimiza demokrasia. Hivi sasa, "awamu ya pili ya kulinda amani" ni tofauti sana na ile ya kwanza.

    "Operesheni za zamani za kulinda amani huwa zinafanyika wakati migogoro kati ya nchi haiwezi kutatuliwa, na vikosi vya kulinda amani hutumwa na Umoja wa mataifa kwenye maeneo yenye migogoro kusimamia usitishaji wa vita. Operesheni za sasa huwa zinatokana na migogoro ya ndani ya nchi fulani, na walinzi wa amani wa Umoja wa mataifa wanatekeleza majukumu ya kulinda utaratibu wa jamii. Katika hali ya pili iliyotajwa, uwekezano wa kutokea mapambano ni mkubwa, ndiyo maana ni hatari zaidi. Tumeona kuwa ndani ya miezi miwili tu, walinzi amani watatu wa China waliuawa au kujeruhiwa, ni kutokana na hatari hiyo."

    Japo kuna walinzi amani wa China waliojitoa muhanga katika shughuli za kulinda amani, China inaendelea kuunga mkono kithabiti juhudi za Afrika kutimiza amani na usalama. Kwa mujibu wa utaratibu wa mpango wa ushirikiano wa amani na usalama kati ya China na Afrika ulio chini ya Baraza la Usalama kati ya China na Afrika, na kuwa nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya utaratibu wa amani na usalama ya Afrika. Bw. Zhou amesema China ina nia na ina uwezo wa kutoa mchango zaidi, kwa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

    "Kwanza, tuna nia thabiti ya kisiasa, yaani kuongeza ushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa mataifa. Tukilinganishwa na nchi nyingi zilizojitolea, pia wanashiriki kwenye operesheni za kulinda amani, lakini hawana dhamira ya kuongeza ushiriki kwenye shughuli hizo. Pili, wanajeshi wa China wana sifa nzuri. Nidhamu na kufuata kwao taaluma vyote vimesifiwa na Umoja wa mataifa na nchi walizotekeleza majukumu. Tatu ni kwamba jeshi la China lina vifaa vizuri vya kisasa. China ikiwa ni nchi kubwa zaidi ya viwanda duniani, inaweza kutengeneza karibu bidhaa zote zinazohitajika, vikiwemo vifaa vya kijeshi. Vifaa tulivyonavyo sasa ni zaidi ya kuliko mahitaji ya kulinda amani. Unachohitaji sasa Umoja wa Mataifa, ni vikosi vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu. China ndiyo ni nchi yenye sifa hizo tatu, tuseme ni sifa za kipekee. Kwa hivyo naona, ni hakika kwamba katika siku zijazo, China itatoa mchango mkubwa zaidi kwenye shughuli za kulinda amani duniani."

    Rais Xi Jinping wa China amesema "China na Afrika ni nguvu muhimu za kulinda amani na utulivu na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia. Tuna sababu, wajibu na uwezo wa kufanya kazi kubwa zaidi katika mambo ya kimataifa na kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi kwa ajili ya kujenga uhusiano wa aina mpya wa kimataifa wenye msingi wa kutafuta ushirikiano wa kusaidiana. Inaaminika kuwa ushirikiano kwenye masuala ya amani na usalama kati ya China na Afrika utasonga mbele na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zitazidi kuboreshwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako