• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yabeba majukumu ya kulinda amani duniani

  (GMT+08:00) 2018-05-29 16:56:48

  Leo ni siku ya maadhimisho ya miaka 70 tangu Umoja wa Mataifa uanzishe operesheni za kulinda amani. Hadi mwaka huu, China imeshiriki kwenye operesheni hizo kwa miaka 28. Ikiwa moja ya nchi kubwa, China inaendelea kubeba majukumu ya kulinda amani duniani.

  Kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za kulinda amani duniani uliofanyika tarehe 28 Septemba mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China alifafanua mawazo ya China kuhusu operesheni za kulinda amani, akisema amani ni matumaini ya pamoja ya binadamu wote, operesheni za kulinda amani zinaleta imani na matumaini ya amani kwa watu wanaoathiriwa na migogoro. Alitangaza kuwa China itajiunga na mfumo wa maandalizi ya nguvu za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, kwa kujenga kikosi cha kudumu cha polisi cha kulinda amani, na kikosi cha maandalizi chenye watu 8,000. Hadi kufikia mwezi Septemba mwaka jana, China ilikuwa imetimiza ahadi hiyo.

  Katika miaka kadhaa iliyopita, China imeharakisha kushiriki zaidi operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Wakati wa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, wanajeshi wa China walijenga kituo cha matibabu kwa siku 28 mfululizo wakikabiliwa na hatari ya kuambukizwa. Katika sehemu yenye mapambano makali nchini Sudan Kusini, wanajeshi wa China waliwaokoa wafanyakazi 7 wa Umoja wa Mataifa. Wakati wa majira ya joto karibu nyuzi 50 sentigredi, wanajeshi wa China walijenga hospitali ndani ya miezi minne nchini Mali.

  Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka 28 iliyopita tangu China ianze kushiriki kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa mwaka 1990, China imetuma wanajeshi zaidi ya elfu 35 kwenye operesheni 24 za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Hivi leo kuna takriban wachina 2,500 wanaotekeleza majukumu ya kulinda amani nje ya China, na idadi hiyo inashika nafasi ya kwanza ikilinganishwa na nchi nyingine wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Pia China inachangia asilimia 10 ya matumizi ya fedha katika kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, na kuchukua nafasi ya pili baada ya Marekani.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres aliipongeza China kwa kutoa mchango muhimu kwa ajili ya operesheni za kulinda amani za umoja huo. Alisema, "China ni nguzo muhimu la kulinda amani duniani, haswa wakati dunia inapokabiliwa na changamoto kubwa. Si kama tu China imetuma watu wengi kwa ajili ya operesheni za kulinda amani, bali pia inafanya kazi muhimu kwa kuusaidia Umoja wa Mataifa kuboresha utaratibu na uwezo, na kuongeza ushirikiano katika operesheni hizo."

  Kutoka ahadi hadi kuchukua hatua halisi, China imeonesha nia ya kuwajibika kama nchi kubwa duniani, pia imethibitisha nia na udhati katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu. Rais Xi alisema, "Dunia ni kubwa, na ina matatizo mengi. Jumuiya ya kimataifa inatarajia sauti na hatua halisi za China. China itawasaidia watu wenye matatizo kadiri iwezavyo. Pia natumai jumuiya ya kimataifa itashirikiana vizuri kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako