• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Umoja wa Mataifa wasema China inatoa suluhisho la matatizo yanayoikabili dunia

    (GMT+08:00) 2018-05-29 18:14:29

    Maofisa wa Umoja wa Mataifa wamesema China inatoa suluhisho za changamoto zinazoikabli dunia, kama vile kudumisha amani na usalama, maendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema, China imechukua nafasi yake katika uongozi wa dunia na kuwa msingi wa mfumo wa pande nyingi. Amesema wakati China inapitia mabadiliko makubwa ya maendeleo ya uchumi, ushiriki wake katika uongozi wa dunia umekuwa wazi zaidi kwa uchumi na maendeleo ya dunia kwa ujumla.

    Pia Katibu Mkuu huyo amesema, China imeshikilia ahadi yake ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), sio tu kwa ngazi ya China, lakini pia katika ushirikiano na nchi nyingine, hususan zinazoendelea.

    Naye naibu mkuu wa Ofisi ya Ushirikiano wa Kusini – Kusini ya Umoja wa Mataifa Wang Xiaojun amesema, maendeleo ya kasi katika miaka 40 tangu kuanzishwa kwa sera ya mageuzi na kufungua mlango yameifanya China kuwa kiongozi katika kuboresha Ushirikiano wa Kusini – Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako