• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa NATO asisitiza kushikilia sera ya pamoja ya ulinzi

    (GMT+08:00) 2018-05-29 18:18:14

    Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema, ingawa bado kuna tofauti lakini nchi za NATO zitaendelea kutekeleza sera ya pamoja ya ulinzi naa kukabiliana na changamoto.

    Akishiriki kwenye mkutano wa majira ya Mchipuko wa NATO mjini Warsaw, Bw. Stoltenberg amesema, katika miezi ya hivi karibuni, nchi za NATO zimetofautiana katika masuala muhimu kama vile, makubaliano ya hali ya hewa ya Paris na makubaliano ya suala la nyuklia la Iran. Amesema, nchi hizo zitafanya mazungumzo kuhusu uhusiano na Russia na ushirikiano kati ya NATO na Ulaya katika mkutano ujao utakaofanyika mwezi wa 7 mjini Brussels.

    Bw. Stoltenberg pia amesema, ingawa uhusiano kati ya NATO na Russia hautaboreshwa ndani ya muda mfupi, lakini pande hizo mbili zinapaswa kuendelea na mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako