• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Nembo ya Rwanda kwenye jesi ya Arsenal yawa gumzo Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-05-29 18:47:10

    Sekta ya Utalii nchini Rwanda itapata ongezeko kubwa la idadi ya watalii kutoka Uingereza na nchi nyingine za bara Ulaya.

    Hii imeshuhudiwa kutokana na gumzo la mashabiki kutoka nchi tofauti ulaya kuambatana na nembo ya Visit Rwanda ama tembea Rwanda kwenye mkono wa shati la Arsenal.

    Juhudi za wizara ya utalii ya Rwanda kufanikisha makubaliano ya klabu hiyo ya soka yenye mashabiki wengi duniani zimezaa matunda.

    Rwanda inatarajia kupokea ongezeko la watalii kwani Arsenal itavaa nembo hiyo kwa miaka mitatu na hivyo kutoa fursa kwa watu wengi kutaka kufahamu nchi hiyo.

    Rwanda imepewa fursa hiyo kutokana na mabadiliko yaliopatikana baada ya vita vya kimbari vilivyofanyika kwaka 1994.

    Kwa sasa ni nchi inayokuwa kwa kasi zaidi kiuchumi Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako