• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UGANDA:Muungano wa Ulaya watoa bilioni 45 kuimarisha uvuvi Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-05-29 18:48:35

    Muungano wa ulaya EU,umetoa shilingi bilioni 45 kusaidia uzalishaji wa samaki katika nchi ya Uganda ,Kenya na Tanzania.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko amesema fedha hizo zitatumika kuboresha uvuvi katika maeneo ya Ziwa Victoria.

    Nchini Uganda biashara ya Samaki inatumika pakubwa kama tegemeo la uchumi kwa mauzo ya nchi za nje lakini hadi sasa uzalishaji wa samaki upo hafifu.

    Mradi huo wa miaka 5 utahusishwa kukabiliwa kwa changamoto za uvuvi ili kufikia malengo ya kuongeza idadi ya samaki kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa EU katika katika Afrika mashariki Roeland Van Geer.

    Usaidizi huo unajiri baada ya viwango vya samaki kutoka Ziwa hilo kuporomoka kwa kiasi kikubwa sana katika miaka ya hivi karibuni.

    Aidha mradi huu unalenga kuiua kipato cha wavuvi .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako