• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania kushirikiana na sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2018-05-29 18:53:37

    Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika malengo ya kupunguza maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)/Ukimwi na Kifua Kikuu kufi kia 2020.

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema hayo jijini Dar es Salaam juzi katika uzinduzi wa Mradi wa Amref Health Africa wa kupambana na Ukimwi na Kifua Kikuu unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Global Fund.

    Mradi huo wa Amref umeidhinishwa fedha zaidi ya Sh bilioni 55.2 kwa ajili ya kuibua na kutibia VVU na kifua kikuu, unatarajia kufikia jumla ya mikoa 15 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara,Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tanga na Ruvuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako