• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yazitaka nchi za Afrika kutumia teknolojia kufanya mageuzi ya kilimo

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:14:00

    Benki ya dunia imezitaka nchi za Afrika kutumia teknolojia ambayo imesema ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kilimo barani Afrika.

    Mchumi mwandamizi wa Benki ya dunia Bw. Ladisy Chengula, amesema bara la Afrika lina nafasi nzuri ya kuendeleza usalama wa chakula kupitia data sahihi zinazopatikana kwa teknolojia za kisasa.

    Bw. Chengula amesema katika miaka ya hivi karibuni uzalishaji wa kilimo barani Afrika umeongezeka, hata hivyo bara la Afrika bado liko nyuma ikilinganishwa na maeneo mengine.

    Bw. Chengula ametolea mfano wa matrekta ya Hello, ambayo wakulima wa Nigeria na Kenya wanaweza kukodi kwa kutumia simu zao, na mazao ya kilimo kwa baadhi yao yameongezeka kwa asilimia 200. Amezipongeza Kenya, Rwanda na Uganda kwa kuongoza matumizi ya teknolojia katika sekta ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako