• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi wa UN aeleza wasiwasi kuhusu ya hali ya Idlib, Syria

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:17:09

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw. Mark Lowcock ameeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama na kibinadamu kwenye eneo la Idlib, Syria. Amesema wakazi wa Idlib na wakimbizi waliokimbilia eneo hilo wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu kutokana na mashambulizi ya anga, mapambano kati ya makundi, msongamano wa watu na ukosefu wa huduma za kimsingi. Kabla ya hapo, mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Syria Bw. Staffan de Mistura alitahadharisha kuwa kama yaliyotokea Ghouta mashariki yatarudia Idlib, matokeo yatakuwa mabaya mara sita zaidi, na watu milioni 2.3 wataathirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako