• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatathmini hasara zinazotokana na mvua kubwa

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:29:52

    Serikali ya Tanzania imesema imeanza kutathmini hasara za mali na miundombinu zilizosababishwa na mvua kubwa inayoendelea nchini kote.

    Naibu waziri wa kazi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Bw Elias Kwandikwa ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa vipaumbele vya tathmini hiyo ni kuchunguza kiwango cha uharibifu wa barabara na madaraja kutokana na mvua hiyo.

    Amesema tathmini hiyo inayofanywa na mamlaka ya barabara ya Tanzania TANROADS, itakayotaja kiasi cha fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukarabati barabara zilizoharibiwa.

    Mvua kubwa iliyoanza kunyesha mwezi Machi imesababisha vifo vya watu zaidi ya 20 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Tabora na visiwani Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako