• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yaahidi dola za kimarekani milioni 2.7 ili kuzisaidia jamii zilizoathiriwa na kimbunga Somalia

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:51:27

    Umoja wa Mataifa umeahidi kutoa dola za kimarekani milioni 2.7 ili kuzisaidia jamii za Somaliland zilizoathiriwa na kimbunga kilichosababisha vifo vya watu zaidi ya 25 na wengine maelfu kukimbia makazi yao.

    Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bw. Peter de Clercq, amesema ni lazima kuchukua hatua za kukabiliana na mchanganyiko wa maafa ya dhoruba, mafuriko na ukame, ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya muda mfupi na ya muda mrefu.

    Kutokana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, kimbunga cha Sagar lilichokaribia Pembe ya Afrika kimewaathiri vibaya watu laki 1.6, na kusababisha vifo vya makumi ya watu, pia kimeharibu vibaya miundo mbinu na kuleta hasara kubwa kwa uchumi, hasa kwa wafugaji wanaotegemea njia za jadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako