• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN akaribisha mkutano wa Paris kuhusu Libya

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:51:55

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Libya Bw. Ghassan Salame amekaribisha mkutano uliofanyika huko Paris kuhusu suala la Libya. Vyama vya siasa nchini Libya vimehudhuria mkutano huo na kujadili njia za kutatua msukosuko wa kisiasa nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya inasema, Bw. Salame ameishukuru Ufaransa na jumuiya ya kimataifa kwa kuiunga mkono Libya kutimiza umoja na utulivu.

    Mkutano huo wa siku moja umetoa taarifa ukisema, pande mbalimbali nchini Libya zimefikia mwafaka kuhusu kufanya uchaguzi wa kuaminika wa rais na wabunge tarehe 10 Desemba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako