• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu watoa wito kuwalenga zaidi vijana katika mapambano dhidi ya Ukimwi Afrika

    (GMT+08:00) 2018-05-30 09:52:46

    Wataalamu wa afya wamesema juhudi za kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi barani Afrika zinapaswa kuwalenga zaidi vijana kutokana na kuwa wao ndio wako hatarini zaidi kutokana na kukabiliwa na shinikizo toka wa vijana wenzao, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na ulevi.

    Wataalamu hao wametoa wito huo katika Warsha ya 12 ya kimataifa kuhusu UKIMWI iliyofunguliwa Jumanne huko Kigali, Rwanda.

    Profesa Elly Katabira wa Chuo Kikuu cha Makerere amesema, viongozi wa Afrika na watunga sera wanapaswa kufanya juhudi zaidi katika kuwalinda vijana na kuwawezesha kujilinda kiafya.

    Serikali ya Sudan Kusini na Shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS walikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kupambana na Ukimwi miongoni mwa vijana. Serikali ya Afrika Kusini vilevile imetangaza kuwa inafanya juhudi kubwa ili kuhakikisha sekta zote za jamii zinashiriki katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako