• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yamwachia kiongozi mashuhuri wa waasi na wengine 575

    (GMT+08:00) 2018-05-30 10:13:05

    Ethiopia imemwachia huru kiongozi mashuhuri wa waasi Andargachew Tsige na wengine 575, kwa ajili ya kutimiza mwafaka na maafikiano ya kitaifa.

    Bw. Tsige, raia wa Uingereza mwenye asili ya Ethiopia ametumikia kifungo gerezani tangu mwaka 2014, kwa makosa ya kuongoza kundi haramu la waasi la Ginbot 7 lenye makao makuu nchini Eritrea, nchi adui mkubwa wa Ethiopia.

    Watu wengine 575 wanaotumikia vifungo magerezani kutokana na makosa mengine mbalimbali, pia wameachiwa huru.

    Kuachiwa kwa wafungwa hao ni sehemu ya ahadi za serikali ya Ethiopia ya mageuzi ya kisiasa na utawala bora.

    Tangu waziri mkuu mpya wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed aingie madarakani Aprili 2, maelfu ya wafungwa wakiwemo watu mashuhuri wa upinzani na wanaharakati wameachiwa huru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako